,

Heshima Quotes

Quotes tagged as "heshima" Showing 1-18 of 18
Enock Maregesi
“Familia yako haikusaidii chochote katika mipango ya takdiri yako. Hii inasikitisha sana. Unajitahidi kila siku kuwafurahisha watu unaowapenda na watu wako wa karibu. Kila ukijitahidi kupata kibali cha watu unaishia kudharaulika na kuonekana mjinga asiyekuwa na maana. Sikiliza mazungumzo ya ndani ya moyo wako. Wapendwa wako watakukubali kama mtu hodari asiyekata tamaa, na tena watakuheshimu kutokana na tabia zako hizo. Mabadiliko haya ya kifikra hayatatokea haraka kama unavyofikiria. Yatachukua muda. Hivyo, kuwa mvumilivu. Wakati huohuo, endelea kucheza ngoma uliyoianzisha mwenyewe, endelea na mipango yako kama akili yako inavyokutuma.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nilijifunza toka awali umuhimu wa kushindwa katika maisha ijapokuwa nilijitahidi sana, na nilipoendelea kushindwa niliweka nadhiri ya kufanya kitu kimoja kilicholeta maana zaidi katika maisha yangu nacho ni uandishi wa vitabu. Uandishi wa vitabu ndicho kitu pekee nilichokiweza zaidi kuliko vingine vyote na kuanzia hapo Mungu aliniweka huru. Nilijua mimi ni nani. Nilijua kwa nini nilizaliwa. Nilijifunza falsafa ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko nilivyoikuta – kwa sababu hata mimi nilikuwepo – na falsafa ya kushindwa si hiari. Maarifa hayo yakafanya niwe na heshima na upendo kwa watu wote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Heshima hujengwa kwa hekima, haijengwi kwa misuli.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wakati mwingine tukitaka kutambulika hatuna budi kuweka mbele aibu ya heshima yetu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukitaka kutambulika usione aibu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu alimpa kila mmoja wetu vipawa na vipaji vya pekee kwa ajili ya huduma yake. Kazi yake kwetu hapa duniani ni kutumia vipawa na vipaji vyetu kwa ajili ya huduma ya watu wengine. Kila mmoja wetu ana kitu fulani anachoweza kutoa kwa ajili ya mtu mwingine mwenye shida. Tunaweza kutoa pesa zetu na muda wetu kwa watu maskini. Tunaweza kuwa marafiki kwa watu wapweke au watu wasiojiweza kiafya. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea kwa ajili ya mabadiliko ya watu wengine. Tunaweza kuwa wasuluhishi wa migogoro ya amani. Tunaweza kuwa na upendo usiokuwa na masharti yoyote kwa familia zetu. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea au kazi za kuajiriwa kwa uadilifu, uaminifu, heshima, na upendo kwa wengine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tupo watu takriban bilioni saba katika dunia hii. Kila mtu ni wa kipekee. Mathalani, wewe ni tofauti na baba yako au mama yako au mtu mwingine yoyote yule. Kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Kila mtu ana nafasi ya kwake mwenyewe aliyopangiwa na Mungu hapa duniani. Haijalishi wewe ni mwanamke au mwanamume, mweupe au mweusi, mfupi au mrefu, mzuri au mbaya, una nafasi katika nchi na dunia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuamka, kufumbua macho na kuujua ukweli. Tafuta maarifa katika Biblia kama wewe ni Mkristo. Tafuta maarifa katika Kurani kama wewe ni Mwislamu. Tafuta maarifa katika Yoga kama wewe haumwamini Mungu. Ukishaamka na kuujua ukweli, ukishapata nafasi katika nchi yako, kuwa kiongozi na mkarimu kwa wenzako. Jifunze kutoka kwa wengine ndani na nje ya tasnia yako. Usiwe mchoyo wa maarifa. Kuwa mwadilifu. Ukifanya hivyo utafanikiwa zaidi, utaipa heshima tasnia yako, na utaacha alama katika dunia baada ya kuondoka. Kuacha alama katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuacha alama katika dunia acha alama katika nchi yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mheshimu sana mtu aliyekupandisha juu kwa sababu utakaposhuka ndiye atakayekupokea, ijapokuwa unaweza usishuke kabisa au unaweza kushuka ukapokelewa na mtu mwingine baki, kwa kudura za Mwenyezi Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi hivi ndivyo wanavyoapishwa na kuikana imani ya Kikristo: Mwanafunzi hupelekwa kilingeni katika siku maalumu kuonana na Shetani, pamoja na jopo la wachawi. Shetani hutokea katika mwili wa hewa, mwili uliochanganyikana na hewa na mvuke mzito, wa mwanamume na kuwasihi waishikilie imani yao kwake kwa mioyo yao yote, huku akiwaahidi utajiri na maisha marefu kama hawatamkana. Kisha wachawi wanampendekeza mwanafunzi kwa Shetani. Shetani humuuliza mwanafunzi kama yuko tayari kuikana imani yake, kuachana na Ukristo na kutokumwabudu Mwanamke Aliyebarikiwa Kuliko Wanawake Wote Duniani Maria Magdalena, na kutoziheshimu sakaramenti za aina zote. Mwanafunzi atakapokubaliana na masharti hayo, Shetani atanyoosha mkono wake na kumsihi mwanafunzi anyooshe wa kwake. Kwa mkono wake mwenyewe, mwanafunzi ataapa na kuweka agano na Shetani mbele ya jopo la wachawi.

Baada ya hapo bila kuchelewa Shetani ataendelea na kusema kuwa hicho kiapo hakitoshi. Lakini mwanafunzi atakapouliza afanye kitu gani cha ziada, Shetani atahitaji kiapo kifuatacho kwa heshima yake na kwa heshima ya mashetani wote: Mwanafunzi ajikabidhi kwa Shetani kwa mwili na kwa roho yake yote daima dawamu, na afanye kila awezalo kuleta wanafunzi wengine wa kike na wa kiume katika ufalme wake. Kama hiyo haitoshi Shetani ataongeza kuwa lazima mwanafunzi atengeneze mafuta fulani kutokana na mifupa na viungo vya miili ya watoto, hasa watoto waliobatizwa, kwani kwa kufanya hivyo atamtimizia kila kitu atakachokitaka hapa duniani. Hiyo ni njia mojawapo ya kiapo.

Njia nyingine ya kiapo ni kwa wale ambao hawajiamini au wana hofu ya kuonana na Shetani uso kwa uso kilingeni, akiwa na mwili wa kimazingaombwe na sauti ya kutisha kwani Shetani hana mapafu wala hana ulimi. Badala ya kilingeni mwanafunzi hupelekwa kanisani na jopo la wachawi ambapo mbele ya jopo atalazimishwa kuikana imani yake, kumkana Yesu Kristo, kuukana ubatizo na kulikana kanisa zima kwa ujumla wake. Mwanafunzi baada ya hapo atalazimishwa kutoa heshima kuu kwa Mfalme Mdogo, kwani hivyo ndivyo wanavyomwita Shetani ili kumwondolea mwanafunzi hofu, kisha atalazimishwa kunywa supu ya mtoto mchanga waliyemuua akazikwa kisha wakamfukua na kupika viungo vya mwili wake; na dakika hiyo mwanafunzi atapata maarifa, maarifa ya kichawi, kama walimu wake na watarudi nyumbani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Rais wa Tume ya Dunia hakuchaguliwa kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, bali alichaguliwa kuleta mabadiliko katika dunia kama Rais wa Tume ya Dunia kutetea afya na amani ya dunia nzima kwa unyenyekevu na heshima kwa binadamu wenzake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiongozi wa wananchi au wa serikali hapaswi kuchaguliwa au kuteuliwa kwa ajili ya kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, anapaswa kuchaguliwa au kuteuliwa kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika nchi kama kiongozi wa dhima aliyokabidhiwa kwa unyenyekevu na heshima kwa wananchi wenzake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna nguzo saba ambazo hazina budi kuzingatiwa kama unataka kuheshimiwa na kuwaheshimu wengine. Kwanza kabisa jitambue: wewe ni nani na unafanya nini hapa duniani. Halafu, kabla ya kusema jambo lolote kwa mtu yoyote fikiria kwanza maana au madhara ya hilo unalotaka kulisema. Kisha jifunze tamaduni mbalimbali na watendee wengine kama vile unavyotaka kutendewa au kama vile wanavyotaka kutendewa. Jifunze kusamehe na kusuluhisha migogoro katika jamii unamoishi huku ukidumisha heshima na utu kwa binadamu wenzako. Jijengee imani kwa watu, punguza upendeleo, fanya kazi kama timu kwani hakuna ‘mimi’ katika umoja ila kuna ‘sisi’, na jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE kwa manufaa ya wote. Kuwa kiongozi katika kila jambo unalofanya na katika kila kitu unachofanya. Jitahidi kufanya jambo au kitu kwa usahihi kwa kadiri utakavyoweza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Juzi si sawa na jana na jana si sawa na leo na leo si sawa na kesho, na kesho si sawa na keshokutwa. Ongea na watu kwa heshima.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mzazi wako akikwambia kuwa usiwe mkorofi, usivunje sheria za nchi, usiwe na marafiki wabaya, na usiasi dhidi ya serikali, mheshimu kwa kukubali. Akikwambia kuwa uwe mkorofi, uvunje sheria za nchi, uwe na marafiki wabaya, na uasi dhidi ya serikali, mheshimu kwa kukataa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Biblia inatuagiza tuwaheshimu wazazi wetu ili siku zetu zipate kuwa nyingi hapa duniani. Mzazi wako akikutuma kuiba mheshimu kwa kukataa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unapokutana na mtu, kisha mtu huyo haoneshi dalili yoyote ya kutaka kusalimiwa; je, anataka umsalimie au usimsalimie? Ndugu yangu, onesha lugha ya mwili kuonesha utu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mzazi wako akikutuma kufanya jambo jema ukakubali umemheshimu. Akikutuma kufanya jambo jema ukakataa umemdharau. Lakini, mzazi wako akikutuma kufanya jambo baya ukakubali umemdharau. Akikutuma kufanya jambo baya ukakataa umemheshimu. Hivyo, mheshimu mzazi wako katika mambo mema na katika mambo mabaya.”
Enock Maregesi