,

Usalama Quotes

Quotes tagged as "usalama" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kasoro za Uzi zilizofanya zisitumiwe tena na kikosi cha usalama cha rais wa Marekani ni kutokuwa na shabaha imara katika umbali mfupi (hutawanya risasi na huleta madhara makubwa katika umbali mfupi hivyo kuweza kudhuru hata watu wasiokuwa na hatia) na kutokuwa na uwezo wa kutoboa kinga ya risasi dhidi ya magaidi wanaotumia mavazi ya kuzuia risasi, wanaotishia usalama wa rais wa Marekani. Gaidi mwenye mavazi ya kuzuia risasi aliweza kumdhuru rais kwa maana ya USSS kushindwa kumdhibiti. Badala yake, sasa USSS wanatumia FNP90 – zenye uwezo wa kutoboa kinga ya risasi, na ambazo hazileti madhara makubwa katika umbali mfupi na katika umbali mrefu. Bunduki hizi, zenye uwezo wa kubeba risasi 100 katika chemba zake mbili za Kampuni ya Beta ('Century Magazines'), zilitumiwa na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Vijana wa Tume na dhidi ya polisi wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwananchi yeyote mwenye taarifa inayohusu biashara haramu ya madawa ya kulevya aitoe taarifa hiyo kwa mamlaka zinazohusika na alindwe, na mamlaka hizo, kwa zawadi na usalama wa maisha yake.”
Enock Maregesi