,

Msomi Quotes

Quotes tagged as "msomi" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Utajiri una changamoto nyingi. Yesu alisema ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Hakusema msomi. Usiwe mwendanguu. Jikusuru kuujua ukweli.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba utajiri una changamoto nyingi kuupata na kuudumisha pia kuliko usomi na kwamba ukweli ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. Heri msomi kuliko tajiri – Heri yule aliyesoma kuliko tajiri asiyesoma au yule aliyesoma kuliko vile alivyosoma tajiri au tajiri asiyesoma au aliyesoma lakini asiyekuwa na tamaa kabisa na dunia hii ambaye kukosa kwake tamaa na dunia hii kunamfanya msomi. Ndivyo Kristo anavyomaanisha. Si kwamba tajiri hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Yusufu, Daudi, Sulemani, Yehoshafati, Hezekia, Zakayo, Yoana, Susana, na Lidia watauona ufalme wa mbinguni na walikuwa matajiri. Mali zao zilivyozidi hawakuangalia moyoni, hawakuwa na tamaa kabisa na dunia hii, bali walimtumaini Mungu kwa kila kitu walichokuwa nacho. Anaweza. Lakini asiipende dunia bali ayapende mambo ya ufalme wa Mungu kwa moyo wake wote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tajiri asiyesoma lakini anayejali mambo ya ufalme wa Mungu kuliko anavyoijali dunia au yule aliyesoma lakini anayejali mambo ya ufalme wa Mungu kuliko anavyoijali dunia ni msomi. Anaweza kuuona ufalme wa Mungu.”
Enock Maregesi