Nenda kwa yaliyomo

A.Y. (mwanamuziki)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.
Ambwene Yesaya

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Ambwene Alen Yesaya
Amezaliwa 5 Julai 1982 (1982-07-05) (umri 42)
Asili yake Mtwara, Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava, hip-hop
Kazi yake


Ambwene Alen Yesaya (anafahamika zaidi kwa jina la AY; amezaliwa Mtwara, 5 Julai 1982) ni mwanamuziki wa muziki aina ya Komesho, Rap na Hip Hop, mwigizaji na pia mwanamitindo kutoka nchini Tanzania.

AY ametoa nyimbo nyingi maarufu nchini Tanzania, kama vile Raha tu 1-2, Raha Kamili, Machoni kama watu, Binadamu n.k.

AY ambaye anafahamika sana nchini Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi hadi Kusini mwa Afrika. Vile vile alikuwa mwanakikundi wa East Coast Team linaloongozwa na Gwamaka Kaihula aliye maarufu kama King Crazy GK, na mwenzake Khamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Falsafa au Mwana FA. Kundi hilo la Muziki lina maskani yao Upanga jijini Dar es Salaam.

Pia Ambwene Allen Yesaya aliwashikirisha ndugu wawili kutoka Nigeria wanaounda kundi la P-SQUARE.

Albamu Alizotoa

  1. Raha Kamili (2003)
  2. Hisia Zangu (2005)
  3. Habari ndiyo hiyo (2008)

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu A.Y. (mwanamuziki) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.