,

Tabasamu Quotes

Quotes tagged as "tabasamu" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Nukuu ya mwandishi wa vitabu wa Brazili, Paulo Coelho, "Tunapopenda tunajitahidi siku zote kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo. Tunapojitahidi kuwa wazuri zaidi kuliko jinsi sisi wenyewe tulivyo, kila kitu katika maisha yetu kinakuwa kizuri hali kadhalika.", inadhihirisha kikamilifu tabia ambayo bibi yangu (Martha Maregesi) alijitahidi kuwa nayo katika kipindi cha maisha yake yote. Alikuwa mtu mwenye furaha sana. Alikuwa na tabasamu lenye kuambukiza ambalo marafiki na familia yake hawakuweza kujizuia kutabasamu pia alipofurahi nao. Pamoja na kwamba alikumbana na matatizo mengi na bahati mbaya nyingi katika maisha yake, alijulikana kama mtu mwenye upendo na uvumilivu mkubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mapema, kabla ndege haijaondoka na baada ya kuagana na maafisa waliomsindikiza, Nanda aliingia katika ndege na kutafuta namba ya kiti chake. Alivyoiona, alishtuka. Msichana mrembo alikaa kando ya kiti (cha Nanda) akiongea na simu, mara ya mwisho kabla ya kuondoka. Alivyofika, Nanda hakujizuia kuchangamka – alitupa tabasamu. Alivyoliona, kupitia miwani myeusi, binti alitabasamu pia, meno yake yakimchanganya kamishna. Alimsalimia Nanda, harakaharaka, na kurudi katika simu huku Nanda akikaa (vizuri) na kumsubiri. Alivyokata simu, alitoa miwani na kumwomba radhi Kamishna Nanda. Nanda akamwambia asijali, huku akitabasamu. Alikuwa na safari ya Bama kupitia Tailandi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Skandinavia na Maxair kutokea Bangkok; sawa kabisa na safari ya kamishna.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Mbegu tunazopanda leo ni mazao ya msimu ujao. Ukipanda mbegu mbaya utavuna mabaya. Ukipanda mbegu nzuri utavuna mazuri. Ukitenda mabaya leo kesho yako itakuwa mbaya. Ukitenda mazuri leo kesho yako itakuwa nzuri. Okoa kesho leo kwa kupanda mbegu nzuri na kuzimwagilia kwa imani na upendo kwa watu. Mungu ataleta mvua, jua na ustawi wa mazao yako. Panda mbegu ya msamaha kwa maadui zako, uvumilivu kwa wapinzani wako, tabasamu kwa marafiki zako, mfano bora kwa watoto wako, uchapakazi kwa kazi zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, ndoto kwa malengo yako, na uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli. Kila mbegu irutubishwe kwa mapenzi huru yasiyokuwa na masharti yoyote, au mapenzi huru yasiyokuwa na unafiki wa aina yoyote ile. Usifiche vipaji vyako. Ukiwa kimya utasahaulika. Usipopiga hatua utarudi nyuma. Usiwe na hasira, wivu au ubinafsi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini, akiendelea kuwaza na kuangaza, ghafla Murphy aliona kitu kama gari likiwa limesimama kwa mbali. Alisimama na kupata hamu ya kujua. Murphy alianza tena kutembea, lakini sasa akiifuata ile gari, halafu akaongeza mwendo na kukimbia; macho yote yakiwa mbele! Alipofika, karibu na gari ile, hakuminya kifyatulio kumpiga mtu risasi. Alijenga tabasamu na kuongeza mwendo. Gari ilikuwa Ferrari Testarrosa ya Lisa Madrazo Graciano!”
Enock Maregesi, Kolonia Santita