,

Nchi Quotes

Quotes tagged as "nchi" Showing 1-16 of 16
Enock Maregesi
“Biblia pamoja na historia vinatwambia kuwa mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kama mfalme wao alivyokufa, kwa sababu walikataa kukana imani yao juu ya Yesu Kristo.

Mathayo alikufa kwa ajili ya Ukristo nchini Ethiopia kwa jeraha lililotokana na kisu kikali, Marko akavutwa na farasi katika mitaa ya Alexandria nchini Misri mpaka akafa, kwa sababu alikataa kukana jina la Yesu Kristo.

Luka alinyongwa nchini Ugiriki kwa sababu ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo katika nchi ambapo watu hawakumtambua Yesu.

Yohana alichemshwa katika pipa la mafuta ya moto katika kipindi cha mateso makubwa ya Wakristo nchini Roma, lakini kimiujiza akaponea chupuchupu, kabla ya kufungwa katika gereza la kisiwa cha Patmo (Ugiriki) ambapo ndipo alipoandika kitabu cha Ufunuo. Mtume Yohana baadaye aliachiwa huru na kurudi Uturuki, ambapo alimtumikia Bwana kama Askofu wa Edessa. Alikufa kwa uzee, akiwa mtume pekee aliyekufa kwa amani.

Petro alisulubiwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wa umbo la X kulingana na desturi za kikanisa za kipindi hicho, kwa sababu aliwaambia maadui zake ya kuwa alijisikia vibaya kufa kama alivyokufa mfalme wake Yesu Kristo.

Yakobo ndugu yake na Yesu (Yakobo Mkubwa), kiongozi wa kanisa mjini Yerusalemu, alirushwa kutoka juu ya mnara wa kusini-mashariki wa hekalu aliloliongoza la Hekalu Takatifu (zaidi ya futi mia moja kwenda chini) na baadaye kupigwa kwa virungu mpaka akafa, alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo.

Yakobo mwana wa Zebedayo (Yakobo Mdogo) alikuwa mvuvi kabla Yesu Kristo hajamwita kuwa mchungaji wa Injili yake. Kama kiongozi wa kanisa hatimaye, Yakobo aliuwawa kwa kukatwa kichwa mjini Yerusalemu. Afisa wa Kirumi aliyemlinda Yakobo alishangaa sana jinsi Yakobo alivyolinda imani yake siku kesi yake iliposomwa. Baadaye afisa huyo alimsogelea Yakobo katika eneo la mauti. Nafsi yake ilipomsuta, alijitoa hatiani mbele ya hakimu kwa kumkubali Yesu Kristo kama kiongozi wa maisha yake; halafu akapiga magoti pembeni kwa Yakobo, ili na yeye akatwe kichwa kama mfuasi wa Yesu Kristo.

Bartholomayo, ambaye pia alijulikana kama Nathanali, alikuwa mmisionari huko Asia. Alimshuhudia Yesu mfalme wa wafalme katika Uturuki ya leo.
Bartholomayo aliteswa kwa sababu ya mahubiri yake huko Armenia, ambako inasemekana aliuwawa kwa kuchapwa bakora mbele ya halaiki ya watu iliyomdhihaki.

Andrea alisulubiwa katika msalaba wa X huko Patras nchini Ugiriki. Baada ya kuchapwa bakora kinyama na walinzi saba, alifungwa mwili mzima kwenye msalaba ili ateseke zaidi. Wafuasi wake waliokuwepo katika eneo la tukio waliripoti ya kuwa, alipokuwa akipelekwa msalabani, Andrea aliusalimia msalaba huo kwa maneno yafuatayo: "Nimekuwa nikitamani sana na nimekuwa nikiitegemea sana saa hii ya furaha. Msalaba uliwekwa wakfu na Mwenyezi Mungu baada ya mwili wa Yesu Kristo kuning’inizwa juu yake." Aliendelea kuwahubiria maadui zake kwa siku mbili zaidi, akiwa msalabani, mpaka akaishiwa na nguvu na kuaga dunia.

Tomaso alichomwa mkuki nchini India katika mojawapo ya safari zake za kimisionari akiwa na lengo la kuanzisha kanisa la Yesu Kristo katika bara la India.

Mathiya alichaguliwa na mitume kuchukua nafasi ya Yuda Iskarioti, baada ya kifo cha Yuda katika dimbwi la damu nchini India. Taarifa kuhusiana na maisha na kifo cha Mathiya zinachanganya na hazijulikani sawasawa. Lakini ipo imani kwamba Mathiya alipigwa mawe na Wayahudi huko Yerusalemu, kisha akauwawa kwa kukatwa kichwa.

Yuda Tadei, ndugu yake na Yesu, aliuwawa kwa mishale alipokataa kukana imani yake juu ya Yesu Kristo.

Mitume walikuwa na imani kubwa kwa sababu walishuhudia ufufuo wa Yesu Kristo, na miujiza mingine. Biblia ni kiwanda cha imani. Tunapaswa kuiamini Biblia kama mitume walivyomwamini Yesu Kristo, kwa sababu Biblia iliandikwa na mitume.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wananchi wataendelea kuwepo hata kama serikali haitakuwepo. Serikali haiwezi kuwashinda wananchi. Sauti ya umma ni sauti ya Mungu. Serikali haiwezi kumshinda Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali mara nyingi hutegemea ujasusi wa ndani na nje kufanya maamuzi mazito na sahihi ya kuendesha nchi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Afrika isomeshe watu wake, na itumie vizuri mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali zake kwa faida ya jumla ya wananchi wa nchi zake, kusudi baadaye wawe wataalamu wa rasilimali za nchi zao wenyewe, kuepukana na utumwa wa rasilimali. Rasilimali za Afrika zina miiko na masharti yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tupo watu takriban bilioni saba katika dunia hii. Kila mtu ni wa kipekee. Mathalani, wewe ni tofauti na baba yako au mama yako au mtu mwingine yoyote yule. Kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Kila mtu ana nafasi ya kwake mwenyewe aliyopangiwa na Mungu hapa duniani. Haijalishi wewe ni mwanamke au mwanamume, mweupe au mweusi, mfupi au mrefu, mzuri au mbaya, una nafasi katika nchi na dunia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuamka, kufumbua macho na kuujua ukweli. Tafuta maarifa katika Biblia kama wewe ni Mkristo. Tafuta maarifa katika Kurani kama wewe ni Mwislamu. Tafuta maarifa katika Yoga kama wewe haumwamini Mungu. Ukishaamka na kuujua ukweli, ukishapata nafasi katika nchi yako, kuwa kiongozi na mkarimu kwa wenzako. Jifunze kutoka kwa wengine ndani na nje ya tasnia yako. Usiwe mchoyo wa maarifa. Kuwa mwadilifu. Ukifanya hivyo utafanikiwa zaidi, utaipa heshima tasnia yako, na utaacha alama katika dunia baada ya kuondoka. Kuacha alama katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuacha alama katika dunia acha alama katika nchi yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuleta mabadiliko katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuleta mabadiliko katika dunia leta mabadiliko katika nchi yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 2 + 2 = 5. Umoja una sisi (ubinadamu), si mimi (ubinafsi). Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano watakuwa na nguvu ya watu watano! Watakuwa na nguvu ya ziada kufanikisha malengo kama vile kuwa na uwezo wa kusaidia jamii kama timu au kama mtu binafsi, kujenga jengo la ofisi, kutengeneza ziada katika masuala ya uchumi wa kampuni au nchi au wa mtu binafsi, ushindi katika kitu chochote kile, na kadhalika. Mimi ni ubinafsi. Sisi ni ubinadamu. Ubinafsi ni uvivu. Ubinadamu ni uchapakazi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dikteta ni kiongozi anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa na mtu, hasa yule aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki. Dikteta uchwara si dikteta, ni dikteta nusu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hatumtaki kiongozi anayeishi katika mifuko ya mafisadi, tunamtaka kiongozi anayeishi katika ibara za katiba ya nchi. Kitambi bila Yesu ni jipu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wasihi watoto wako kuipenda nchi yao.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kura ni haki yako ya msingi kabisa kwa ajili ya maendeleo yako na ya nchi yako. Ongea na nchi yako. Yaani, chagua kiongozi atakayeweza kukuletea maendeleo. Kama hujachagua mtu, usimlalamikie yule aliyechaguliwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama umechagua mtu akashinda au akashindwa na matokeo yakatangazwa, idadi kubwa ya watu ikakubaliana na matokeo hayo, umeongea na nchi yako na imekujibu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiichukia serikali yako umeichukia nafsi yako. Kwa sababu serikali ndiyo inayoongoza nchi, na nchi ni mwili mmoja.”
Enock Maregesi