,

Maji Quotes

Quotes tagged as "maji" Showing 1-10 of 10
Tomi Adeyemi
You carry all of us in your heart. We shall live in every breath you take. Every incantation you speak.
Tomi Adeyemi, Children of Virtue and Vengeance

Enock Maregesi
“Kuna ndoto za mchana na kuna ndoto za usiku. Ndoto za mchana ni maono ya kile ambacho roho inatamani kuwa. Ndoto za usiku ni maono yanayotokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira; ukiota kuhusu maji, hiyo ni ishara ya siri; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni; ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio. Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani, utakapoamka, mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea; au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua. Ubongo ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni na umetengenezwa na Mungu. Ndoto zinapatikana ndani ya ubongo. Ubongo unapatikana ndani ya ufahamu. Ufahamu mtawala wake ni malaika mwema. Malaika mwema anajua siri ya ndoto. Kila mtu anaota na kila ndoto ina maana yake. Rekodi ndoto zako kila siku kwa angalau mwezi mzima kupata maana halisi ya ndoto hizo, na kujua kwa nini ulizaliwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa ni ya muhimu kwa sababu ya mahitaji ya lazima ya wanadamu kama vile chakula, maji, malazi, elimu, usafi, mavazi, na afya, lakini ni ya maana kwa sababu ya wanawake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Aidha, tunaweza kupata inkishafi kutokana na asili ya miili yetu, matukio fulani ya wakati ujao yana asili yake katika ndoto za binadamu. Ndoto hizo au maono hayo ni ishara ya kile kinachokuja mbele katika maisha ya mtu; kama vile afya, ugonjwa au hatari. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira – unatakiwa kuwa na hekima; ukiota kuhusu mimba na unajifungua, hiyo ni ishara ya kuwa katika mchakato wa kutengeneza wazo jipya – unatakiwa kushukuru; ukiota unaruka angani, hiyo ni ishara ya tumaini – unatakiwa kushukuru; ukiota kuhusu maji au kiowevu kingine chochote kile, hiyo ni ishara ya siri na wakati mwingine ni ishara ya kuwa na matatizo ya kiafya kama utaota kuhusu maji machafu – unatakiwa kuwa msiri na msafi; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni – unatakiwa kuomba; na ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio – unatakiwa kushukuru.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Damu na maji vilitoka katika mbavu za Yesu Kristo kutokana na upungufu wa damu mwilini, hipovolimia, kulikotokana na kuchapwa bakora. Yesu alichapwa bakora arobaini kabla ya kupelekwa Golgotha. Matokeo ya hipovolimia katika mwili wa mtu ni moyo kwenda mbio kusukuma damu iliyopungua, kuzimia kutokana na msukumo wa damu kuwa chini, figo kushindwa kufanya kazi na kiu ya maji.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kabla ya kukata roho mapigo ya kasi ya moyo aliyoyapata Yesu kutokana na mshtuko wa hipovolimia, pia yalisababisha maji kujikusanya katika vifuko vya maji au ute kandokando ya moyo na kandokando ya mapafu. Mkusanyiko huu wa maji kandokando ya moyo hujulikana kama ‘pericardial effusion’ na mkusanyiko wa maji kandokando ya mapafu hujulikana kama ‘pleural effusion’. Hii ndiyo maana baada ya Yesu kukata roho, na askari wa Kirumi kurusha mkuki katika ubavu wake, baada ya kutoboa mapafu na moyo, damu na maji vilitoka katika mbavu za Yesu kama Yohana alivyorekodi katika Injili yake. Mapafu ya Yesu na tumbo la Yesu vilijaa damu na maji. Mkuki ulivyotupwa maji yalitoka katika mapafu ya Yesu na katika tumbo la Yesu, na katika utando unaozunguka moyo wa Yesu, kutokana na kupasuka kwa moyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Damu, mto wa maisha unaotiririsha maji yake mwilini kwa kusukumwa na pampu za moyo na kuchujwa na fizi za mapafu, inaundwa na seli na maji yaitwayo utegili au maji ya damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha oksijeni na virutubisho katika kila sehemu ya mwili, ndani yake kuna roho. Mungu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Ibrahimu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Israeli ijapokuwa mapenzi ya Mungu kwa Israeli yalikwisha baada ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Wana wa Israeli walitoa kafara za damu kwa ajili ya wokovu wa watoto wao wa kwanza na watoto wa kwanza wa wanyama wao nchini Misri. Mungu alitoa kafara ya damu ya Yesu Kristo nchini Israeli kwa ajili ya wanadamu wote duniani. Damu ya mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi, imetiwa wakfu na Mwenyezi Mungu na ina uhusiano mkubwa na ulimwengu wa roho. Ukifunikwa na damu ya mwanakondoo Shetani hatakuona. Shetani asipokuona, utafanikiwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45). Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mnamo mwaka 1957 Rais David Eisenhower wa Marekani (inasemekana) alipewa taarifa usiku mmoja akiwa Washington, D.C., kuhusu chombo cha ajabu kilichoanguka kwenye jangwa la Nevada huko Marekani. Ndani ya chombo kile kulikuwa na ‘aliens’ wawili, nao waliomba kuonana na Eisenhower kuhusu ujumbe waliokuja nao kutoka katika ulimwengu wao.

Bila kuchelewa, Eisenhower alipanda ndege usiku huohuo mpaka Texas. Huko alichukua gari hadi kwenye eneo la kijeshi liitwalo Area 51, ambapo ndipo ule ujumbe wa ulimwengu mwingine ulipokuwa umeshikiliwa.

Mkutano wa aina yake ulifanyika chini ya ardhi, kati ya Rais Eisenhower na hao viumbe wawili wa anga za mbali, chini ya tafsiri ya wanasayansi wa NASA. Walichotaka ni urafiki na dunia yetu, inayogombewa na dunia nyingi za ‘aliens’, kwa mbadala wa teknolojia kadha wa kadha ambazo sisi hatukuwa nazo.

Pande zote mbili zilifikia maafikiano, wao wakitupa teknolojia, sisi tukiwapa uwezo wa kufanya majaribio ya kisayansi kwa binadamu wa dunia nzima. Hivyo kuanzia hapo ‘aliens’ wakawa na uhalali wa kuteka watu katika mazingira ya kutatanisha na kuingilia watu usiku wakiwa wamelala, katika tukio la kiulimwengu wa roho lijulikanalo kama ‘sleep paralysis’.

‘Sleep Paralysis’ ni tukio la ajabu. Mtu anapokuwa amelala mwili wake huonekana kufa ganzi, kiasi kwamba anajihisi hawezi hata kunyanyua mkono. Aghalabu hali hiyo inapotokea maana yake ni kwamba ‘aliens’ wanamchukua huyo mtu, kupitia kwenye paa la nyumba aliyolala, hadi mawinguni katika ndege yao. Ndani ya ndege wanaulaza mwili wa binadamu juu ya kitanda cha upasuaji, na kumfanyia upasuaji, ili kusoma biolojia iliyotumika kuumba wanadamu na kujua kwa nini sisi tuko tofauti na wao. Baada ya hapo wanamrudisha huyo mtu kitandani kwake, ambapo atalala usingizi wa kawaida hadi asubuhi. Atakapoamka hatajua kama alifanyiwa upasuaji.

Wapo mamilioni ya watu duniani waliolalamika kutokewa na ‘aliens’, lakini serikali haziwahi kuilithibitisha hilo. Inavyosemekana, teknolojia za ‘aliens’ zinahifadhiwa na Jeshi la Marekani (Pentagon) na shirika la kijasusi la MAJI au MJ12. MJ12 ni watu 12 hatari zaidi duniani, wakiongozwa na mkurugenzi mkuu wa CIA (anayejulikana kama MJ1).”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mbegu ni neno la Mungu na kudondoka kwake kwenye ardhi si mwisho wa maisha yake. Mambo kadha wa kadha yanaweza kutokea yanayoweza kuathiri ukuaji wa mbegu husika. Nyingine zinaweza kuanguka karibu na njia ndege wakaja wakazila, nyingine zinaweza kuanguka penye miamba pasipokuwa na udongo mwingi wa kutosha, nyingine zinaweza kujifukia ndani kabisa ya ardhi na kupotelea huko kwa miaka mingi, mvua inaweza kunyesha na kuhamisha baadhi ya mbegu kwa kuzisomba na maji. Lakini kwa kuwa maisha yamo ndani ya mbegu, jambo fulani litatokea.”
Enock Maregesi