,

Daniel Yehuda Quotes

Quotes tagged as "daniel-yehuda" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Israeli Daniel Yehuda Ben-Asher Ebenezer, Mhebrania aliyeishi Givat Ram, Jerusalem, na mke wake mrembo Hadara na mtoto wake mzuri Navah Ebenezer, alikuwa Ukanda wa Gaza siku alipopigiwa simu na Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia U Nanda – kutoka Copenhagen kuhusiana na wito wa haraka wa kuonana na Rais wa Tume ya Dunia. Yehuda aliondoka usiku kwenda Yangon, Myama, ambapo alionana na U Nanda na kupewa maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa kuyafuata. Mbali na maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa kuyafuata, Nanda alimkabidhi Yehuda kachero wa Kolonia Santita Mandi Dickson Santana (bila kujua kama Mandi ni kachero wa Kolonia Santita) ili amsindikize mpaka stendi ya mabasi ya Maubin, nje ya Yangon. Baada ya hapo Yehuda alisafiri mpaka Copenhagen ambapo yeye na wenzake walikabidhiwa Operation Devil Cross, ya kung’oa mizizi ya Kolonia Santita duniani kote. Yehuda alifanya kosa kubwa kuonana na kachero wa Kolonia Santita Mandi Santana! Kwa sababu hiyo, sauti na picha ya Yehuda vilichukuliwa, watu wengi walikufa katika miji ya Copenhagen na Mexico City.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ujanja wote ulimwisha Murphy. Ilimbidi kutoboa siri ili adui asizidi kumuumiza. Alilaumu mno kufa wakati alishakula ng’ombe mzima. Alifikiri Mogens na Yehuda walishauwawa kulingana na hasira nyingi za magaidi. Walihakikisha hawafanyi makosa hata kidogo. Alivyomaliza kumhoji, yule adui alizunguka nyuma katika mgongo wa Murphy na kwenda katika dirisha lililokuwa wazi – la mashariki – ambapo aliegemea na kuvuta sigara. Alichungulia kidogo nje kisha akageuka na kuendelea kupata upepo mdogo wa baridi.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Wakati Ford Bronco inatoka katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals S.A de C.V. (kilichomilikiwa na mkurugenzi mkuu wa 'methamphetamine' wa Kolonia Santita mfanyabiashara wa Kichina kutoka Chaling, katika jimbo la Hunan, kusini ya kati ya China, Li Dongyang; na mkurugenzi wa usalama wa Kolonia Santita kutoka Lomas de Chapultepec, Mexico City, Gortari Manuel) Daniel Yehuda na Radia Hosni, waliokuwa wakipiga picha kila kitu kilichokuwa kikiingia na kutoka kiwandani kwa ajili ya ripoti ya upelelezi wao ya baadaye, waliiona. Lakini, hawakujua kama ilikuwa ikienda Varsovia kumuua Murphy na Sajini Mogens.

Bronco ilipofika Varsovia ilisimama kwa fujo mbele ya SUV ya msafara wa Mtoto wa Rais Debbie Patrocinio Abrego, aliyekuwa ndani ya Mgahawa wa Angus akicheza muziki wa 'mariachi' na John Murphy, huku Mogens akilinda usalama wa kamanda wake na usalama wa baa nzima. Kabla majambazi wa Kolonia Santita hawajaleta madhara au fujo yoyote kwa Vijana wa Tume, polisi walifika eneo lile haraka ilivyowezekana! Kwa msaada wa walinzi wa Debbie! Wale majambazi walipekuliwa na kukutwa na bastola moja ya Akdal Ghost, bunduki mbili za AK-47, na picha nne za Vijana wa Tume ndani ya gari yao. Polisi waliwakamata na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Tume ya Dunia kilichopo Zona Rosa, Mexico City.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel 'Yehuda Ben-Asher' Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kitengo cha mauti na utekaji nyara cha Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli (Kidon) kabla ya kujiunga na Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC) huko Oslo, kwa makubaliano maalumu kati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) na Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ghillie ni mavazi yaliyotumiwa na makomandoo wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (Frederik Mogens, Radia Hosni, Daniel Yehuda na John Murphy) kama mbinu ya kujificha kwa kujifananisha na rangi au maumbo ya mazingira ya Msitu wa Benson Bennett, kama afanyavyo kinyonga. Hata hivyo, walivyoingia katika jumba la utawala katika maabara za Kolonia Santita ndani ya Msitu wa Benson Bennett katika mji wa Salina Cruz, Vijana wa Tume walivua suti zao za ghillie; kusudi iwe rahisi kwao kupambana na jeshi binafsi la Kolonia Santita, liitwalo 'autodefensa'.”
Enock Maregesi