,

Damu Quotes

Quotes tagged as "damu" Showing 1-11 of 11
Enock Maregesi
“Potassium Cyanide si hatari inapokuwa nje. Ni hatari inapojichanganya na asidi za tumboni ambapo hubadilika na kuwa gesi ya 'hydrogen cyanide'. Gesi ya 'hydrogen cyanide' ni miongoni mwa sumu hatari zaidi ulimwenguni. Mtu akimeza kidonge cha 'cyanide' atapata madhara makubwa. Kichwa chake kitamuuma hapohapo na atachanganyikiwa akili. Ngozi yake itakuwa nyekundu, kwa sababu damu yake itakuwa nyekundu zaidi – kutokana na kuzidi kwa oksijeni katika damu. Mwili hautakuwa na uwezo tena wa kuchukua oksijeni kutoka katika damu ili uitumie, kwa hiyo damu itazidi kuwa na oksijeni zaidi. Atapumua kwa shida. Mapafu yake yatafanya kazi vizuri lakini mwili wake hautakuwa na uwezo wa kutumia oksijeni yoyote – hivyo atadhani ana matatizo katika mfumo wake wa kupumua. Atazimia. Yaani, oksijeni haitafika kwenye ubongo. Atapata kifafa na atatapika nyongo. Ubongo wake utashindwa kufanya kazi na atakuwa mahututi ndani ya sekunde kumi! Baada ya hapo moyo wake utasimama kufanya kazi, na atafariki dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lengo kuu la Kolonia Santita kuuza madawa hayo ni kuwafadhili askari wa msituni wa Kolombia (magorila wa vyama visivyokuwa rasmi vya kisiasa au vyama haramu vya kisiasa) kushika hatamu za uongozi wa Kolombia, kwa makubaliano ya Kolonia Santita kutawala biashara ya kokeini ya taifa hilo la Amerika ya Kusini. WODEA lazima ilizuie Shirika la Madawa ya Kulevya la Kolonia Santita kuuza madawa hayo kwa gharama yoyote ile, pesa au damu, kutetea afya na amani ya dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiua mtu damu yake itakusuta maisha yako yote! Itaongea na wewe ikikulaumu milele!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Uwezekano wa watoto wa ukoo mmoja kuoana ni mkubwa kwa sababu damu ina nguvu ya uvutano. Kuhakikisha kwamba familia zinafahamiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ni jukumu la wazazi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Damu na maji vilitoka katika mbavu za Yesu Kristo kutokana na upungufu wa damu mwilini, hipovolimia, kulikotokana na kuchapwa bakora. Yesu alichapwa bakora arobaini kabla ya kupelekwa Golgotha. Matokeo ya hipovolimia katika mwili wa mtu ni moyo kwenda mbio kusukuma damu iliyopungua, kuzimia kutokana na msukumo wa damu kuwa chini, figo kushindwa kufanya kazi na kiu ya maji.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Damu, mto wa maisha unaotiririsha maji yake mwilini kwa kusukumwa na pampu za moyo na kuchujwa na fizi za mapafu, inaundwa na seli na maji yaitwayo utegili au maji ya damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha oksijeni na virutubisho katika kila sehemu ya mwili, ndani yake kuna roho. Mungu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Ibrahimu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Israeli ijapokuwa mapenzi ya Mungu kwa Israeli yalikwisha baada ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Wana wa Israeli walitoa kafara za damu kwa ajili ya wokovu wa watoto wao wa kwanza na watoto wa kwanza wa wanyama wao nchini Misri. Mungu alitoa kafara ya damu ya Yesu Kristo nchini Israeli kwa ajili ya wanadamu wote duniani. Damu ya mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi, imetiwa wakfu na Mwenyezi Mungu na ina uhusiano mkubwa na ulimwengu wa roho. Ukifunikwa na damu ya mwanakondoo Shetani hatakuona. Shetani asipokuona, utafanikiwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Siku ya kwanza dhambi ya kwanza ilipotendwa Mungu alitoa kafara ya kwanza ya wanyama kwa ajili ya wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa. Adamu na Hawa walikuwa uchi, baada ya kutenda dhambi, Mungu akawalaani lakini akawapa uwezo wa muda mfupi wa kutubu dhambi zao ili awasamehe! Kutokana na ngozi za wanyama hao walipata mavazi na kutokana na damu ya wanyama hao walipata fursa ya kuishi na kutubu dhambi zote walizozitenda. Bila hivyo wasingepata muda wa kusamehewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama damu haina maana kwa nini Mungu anaipenda? Kama damu haina maana kwa nini Shetani anaipenda? Mungu ni roho, Shetani ni roho, lakini damu ni kitu kinachoonekana kwa macho. Kwa nini damu ni kitu cha muhimu kiasi hicho kwa Mungu na kwa Shetani pia? Damu ni pato la ziada la ufunuo wa kiroho. Yaani, damu ni sehemu ya ulimwengu wa roho. Mungu ndiye aliyetengeneza damu kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe, hata Shetani hajui kwa asilimia mia umuhimu wa damu katika ulimwengu unaoonekana na katika ulimwengu usioonekana. Damu ina uwezo wa kuzuia mapepo kutoka kuzimu yasiharibu mipango ya maisha ya watu na ina uwezo wa kuondoa dhambi. Kafara ya damu inapotolewa inaimarisha uhusiano kati ya mtu na ulimwengu wa roho. Roho unayoitolea kafara inasikiliza shida zako papo hapo na kila unachoomba aghlabu kinatekelezwa. Ukitoa kafara kwa ajili ya Shetani, Shetani atasikiliza shida zako. Ukitoa kafara kwa ajili ya Mungu, Mungu atasikiliza shida zako. Tatizo kubwa la mwanadamu ni dhambi! Jibu la tatizo hilo ni damu ya Yesu Kristo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani anapenda damu kumtumia Mungu kwa faida yake kama vile Mungu anavyomtumia Shetani kwa faida yake. Mungu anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu, na Shetani anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Mungu anaishi ndani ya damu na damu ina nguvu kuliko Shetani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kusudi mimba itungwe lazima kuwepo na kromosomu X na kromosomu Y. Kromosomu ni nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni au DNA, ambazo hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbe hai kutoka kwa mama na baba wa kiumbe hicho. Kwa upande wa Yesu Kristo, katika hali ya kawaida, kromosomu X ilitoka kwa Maria Magdalena na kromosomu Y ilitoka kwa malaika Gabrieli. Yesu alikuwa Myahudi lakini Kristo ni Mungu. Yesu Kristo alikuwa binadamu kama sisi, lakini alikuwa na utukufu na alikuwa na damu ya Mungu iliyotakasika. Damu kama hiyo ndiyo inayotiririka katika miili ya kila mmojawetu ijapokuwa ni damu ya Adamu, ambayo bado haijatakaswa. Damu ya Yesu si kitu kidogo. Ilipomwagika msalabani ilifunika dunia nzima. Ndiyo maana tukasamehewa. Bila damu hiyo, bila utukufu huo wa Mungu, hakuna binadamu atakayeokolewa, hakuna pepo atakayeondolewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu anaishi ndani ya damu, maisha ya Mungu yalikuwa yanaishi ndani ya mwili wa Yesu Kristo, anaishi ndani ya miili yetu. Unapokula damu, unapokunywa damu, unakula, unakunywa sehemu ya Mungu aliyekuumba.”
Enock Maregesi